TOFAUTI KATIKA UBONGO WA MWANAUME NA MWANAMKE

Tofauti ya ubongo wa mwanamke na wa mwanaume. (Human brain analysis) - By Giningi Siyabonga (Braza Joni)

1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume hawezi.

2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.

3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanaume uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo wao ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso. Guys, next time ukiwa unamdanganya msichana ni better mkiwa hamko uso kwa uso.

4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbali na kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.

5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.

6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.

0 Response to "TOFAUTI KATIKA UBONGO WA MWANAUME NA MWANAMKE"

Post a Comment